Kimenuka...Vijana Wawili Wanusurika Kifo Wakijaribu Kupora Duka la Kubet Dar



Dar es Salaam. Vijana wawili wanaodaiwa kuwa ni wezi wanusurika kuuawa na wananchi, baada ya kuvamia ofisi ya michezo ya kubahatisha (Premier bet) eneo la Mwenge.

Vijana hao ambao walifika kama wateja wanahitaji huduma, walianza kumshambulia mhasibu kwa kumpiga na jiwe kichwani huku mwingine alijaribu kuvunja sefu zilizokuwa na fedha bila mafanikio.

Akizungumza na Mwananchi Digital leo Jumanne Septemba 27, akiwa amelazwa katika Zahanati ya Mwenge mhasibu wa ofisi hiyo Mwanahija Abdalh, amesema vijana hao waliofika muda mfupi baada ya yeye kufungua.

"Saa tatu kama na nusu aliingia mteja mmoja ambaye sikumfahamu, wakati huo nilikuwa nahangaika kuweka mtandao sawa.


"Alisimama kidogo na baadae akaondoka na aliporudi alikuwa na mwenzake wakaingia kaunta, nilipomwambia huruhusiwi mtu kuingia huku kumbe alikuwa na jiwe na akaanza kunishambulia kichwani, wakati huo mwenzake akiwa anahangaika kuvunja droo," amesema Mwanahija.

Amesema alifanikiwa kupiga kelele bahati nzuri walipoanza kukimbia watu waliokuwa nje walikuwa wamesikia ndipo walipowakamata wakiwa wanataka kukimbia.

"Kutokana na mshtuko walipokuwa wananipiga nilianguka, kwa bahati nzuri nilishtuka nikawa napiga kelele hata hivyo namshukuru walikamatwa na mimi nikaletwa hospitali," amesema.


Msimamizi wa Goodluck Masawe amesema alipata taarifa akiwa Manzese ndipo na kuchukua pikipiki ambapo alifika baada ya muda mfupi na kukuta waneshadhibitiwa.

“Nilikuta wamepigwa vibaya sana mmoja akiwa amelala nje ya ofisi na mwingine amelala kwa ndani kando ya barabara, hata hivyo nilishukuru Jeshi la Polisi kwa kufika kwa wakati," amesema.

"Baada ya kumpiga walitegemea angepoteza fahamu ili wachukue fedha bahati nzuri waliwahiwa na watu waliokuwa nje"Masawe

Masawe amesema hilo sio tukio lakwanza kutokea kwani wiki iliyopita walivamia nyingine iliyopo Sinza Madukani na kufanikiwa kupora Sh1 milioni.


Alipotafutwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Jumanne Muliro, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema Polisi walifika eneo la tukio na kukuta wananchi wameshawadhibiti ili wasiweze kutoroka.

"Polisi walifika eneo la tukio na kukuta wananchi wamewapiga, kilichofanyika ni kuwachukua na kuwapeleka hospital huku uchunguzi ukuwa unaendelea," amesema Muliro.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad