Kioja Baada ya Jamaa Aliyezikwa Kurejea Nyumbani Akiwa Mzima





Kioja Baada ya Jamaa 'Aliyezikwa' Arejea Nyumbani Akiwa Mzima Miaka 3 Baadaye
Wakaazi wa kijiji cha Kamukuywa nyumbani kwa jamaa aliyerejea nyumbani baada ya kudhaniwa kuwa ameaga dunia. Picha: UGC
Mwanamume huyo aliyetambulika kama Isaac Wanjala alisemekana kuwa alipenda kutoweka na kutokea tena kulingana na familia yake

Kutokana na tabia ya Wanjala kuondoka nyumbani na kurejea, awali familia hiyo haikufadhaika alipoondoka nyumbani 2019 kwenda kazini.

"Kwa muda, hatukuwa tumemwona. Anapoondoka tunasubiri tu hadi arudi nyumbani. Hata hivyo, miezi saba baadaye, tulipokea habari za kuhuzunisha kwamba mwanamume anayefanana na Wanjala ameuawa," mama huyo alisema.



Familia yake ilisema kuwa mwili waliopokea ulikuwa umekatwakatwa kiasi cha kutotambulika.

Mwili huo ulipelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Webuye na baadhi ya jamaa zake waliutanmbua kuwa ni wa mpendwa wao Wanjala.

Hata hivyo mmoja wao alikuwa na shaka juu ya utambulisho wa maiti hiyo.


"Watu walienda katika makafani kuutambua mwili huo. Mwalimu, mfanyabiashara na kakake Wanjala walithibitisha kuwa mwili huo ulikuwa wake na mipango ya mazishi ikaanza," jamaa mmoja alibainisha.

Licha ya mashaka yaliyoibuka, mwili huo ulizikwa 2021 na familia ikasonga mbele na maisha wakianza kumsahau mwanao.

Kufuatia matukio ya ghafla, maiti iliyozikwa itafukuliwa na kupelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Webuye huku uchunguzi ukiendelea.

Polisi wa eneo hilo walithibitisha kisa hicho cha kustaajabisha na kuwataka wakaazi kuwa waangalifu wanapotambua miili ili kuepusha mkanganyiko.


"Tulipokea ripoti kuwa mwanamume mmoja alitoweka na msako ulianzishwa. Msako huo ulisitishwa hata hivyo familia ilipoeleza kuwa ilimpata mwanamume huyo katika hifadhi ya maiti ya Webuye," mkuu wa polisi wa Kimilili Mwita Maroa aliripoti.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad