Kiungo Fundi Yanga Ananukia Fedha Mshahara Wake Gumzo Jangwani



IMEBAINIKA kuwa, kiungo wa Yanga, Mrundi, Gael Bigirimana, alijiunga na timu hiyo kwa dau lililotajwa kuwa ni dola 85,000 ambazo ni sawa na Sh 197,452,450 za Kitanzania na kumfanya kuwa miongoni mwa nyota ghali kikosini hapo.

Kiungo huyo wa zamani wa Newcastle ya England, amejiunga na Yanga msimu huu kwa mkataba wa miaka miwili akiwa mchezaji huru baada ya kuachana na …. Taarifa zinasema kwamba, mbali na dau hilo la usajili, kwa mwezi nyota huyo atakuwa analipwa dola 8,000 ambazo ni sawa na Sh 18,583,760.

Mgawanyiko wa fedha hizo za mshahara kwa wiki analamba dola 2,000 ambazo ni sawa Sh 4,645,940 za Kitanzania. Kwa siku, hesabu zinaonesha kwamba atakuwa anapokea dola 285.7 ambazo ni sawa na Sh 663,673 za Kitanzania, huku kwa saa ikiwa ni dola 11.9, sawa na Sh 27,654.4 za Kitanzania.

Fedha hizo ukija kuziweka kwa mwaka, unapata dola 96,000 sawa na Sh 223,005,120 za kitanzania. Mchaganuo huo unamfanya kiungo huyo kunukia fedha kama watoto wa mjini wanavyosema pindi mtu akiwa na fedha nyingi.

Chanzo chetu kutoka Yanga, kilibainisha kwamba: “Uzuri wa kikosi chetu kwa sasa unachangiwa zaidi na ubora wa mishahara na pesa za usajili ambazo viongozi tuliamua kutumia kuhakikisha tunapata wachezaji wanaojitambua, ndiyo maana utagundua hadi tunainasa saini ya mchezaji mkubwa kama Bigrimana tumepoteza zaidi ya dola 8000.

“Ukiangalia kwa sasa utagundua wazi kabisa mishahara inayolipwa na klabu yetu inawafanya hata wachezaji wenyewe kuwa na utulivu mkubwa maana ni mikubwa, inawafanya hata wao kututumikia bila mashaka.”
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad