KLABU ya Yanga, imeingia mikataba miwili ya Mabilioni na Kampuni ya GSM


KLABU ya Yanga, imeingia mikataba miwili na Kampuni ya GSM ambayo itaifanya timu hiyo kuvuna Sh10.9 bilioni kwa miaka mitano.

Katika hafla hiyo ambayo ilifanyika jijini Dar es Salaam huku ikisimamiwa na wanasheria wa Yanga na GSM, Saimon Patrick na Davis Kato, rais wa Yanga, Hersi Said alisema hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi zake.

Hersi alisema moja ya ahadi zake ni kuifanya Yanga kuimarika kiuchumi; "Leo nasimama hapa kusema kwamba tumekubaliana na GSM, mkataba wa kwanza wa utengenezaji wa jezi na vifaa bilioni wenye thamani ya Sh9.1 bilioni miaka mitano."

Katika ufafanuzi wa mkataba huo, alisema kutakuwa na ongezeko kwa asilimia 10 kwa kila mwaka.

Mkataba wa pili kati ya GSM na Yanga, ulikuwa upande wa udhamini ambapo timu hiyo ya Wananchi itavuna Sh 300 milioni kila mwaka huku kukiwa na ongezeko la asilimia 10.

Awali Yanga ilikuwa ikivuna Sh150 milioni kutokana na udhamini huo ambao uliwafanya GSM kuweka matangazo ya bidhaa zao kwenye jezi.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad