Kocha Matola Ajitetea "Robo Tatu ya Wachezaji Simba Walicheza Chini ya Kiwango cha Kawaida"

 


Kocha Msaidizi wa Simba SC Seleman Matola ametetea maamuzi ya kumtumia muda wote Beki wa Kulia Israel Patrick Mwenda, katika mchezo dhidi ya KMC FC uliomalizika kwa sare ya 2-2.


Miamba hiyo ya Dar es salaam ilipapatuana jana Jumatano (Septemba 07) Uwanja wa Benjamin Mkapa, huku beki Israel Mwenda akigeuka gumzo kutokana na kuonesha kiwango duni.


Kabla ya kuondoka Dar es salaam kuelekea Lilongwe Malawi tayari kwa mchezo wa Kimataifa, Kocha Matola amesema hakuwa na namna nyingine ya kumtoa Mwenda kwa sababu aliyezoeleka kucheza nafasi hiyo (Shomari Kapombe) ni majeruhi.

Hata hivyo Matola amekiri Mwenda alicheza chini ya kiwango na kuigharimu timu kwa kiasi kikubwa, lakini bado hakuacha kutoa lawama kwa wachezaji wengine kucheza chini ya kiwango pia.


“Shomari anaumwa, tulikuwa na beki mmoja wa kulia kitu ambacho hatukuweza kumbadilisha Israel Mwenda. Isra hakuwa na mchezo mzuri lakini karibu robo tatu ya wachezaji hawakuwa na mchezo mzuri. Kama tungeweza kufanya mabadiliko, tungefanya karibu nusu ya timu nzima.” amesema Matola


Simba SC ilikua na wakati mgumu sana katika mchezo huo, baada ya kutanguliwa kwa mabao mawili, lakini juhudi za baadhi ya wachezaji wake ziliwafanya kupata bao la kusawazisha kupitia kwa Mshambuliaji Habib Kyombo aliyeingia dakika za lala salama.


Kwa matokeo hayo Simba SC imerejea kileleni kwa kuwa na alama saba sawa na Young Africans na Mtibwa Sugar, lakini uwiyano wa mabao mengi ya kufunga umeiweka klabu hiyo ya Msimbazi kwenye nafasi ya kwanza.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad