BOSI wa Ufundi wa vikosi vya vijana wa Yanga, Mwinyi Zahera amewagomea mabosi wa Shirikisho la Soka nchini DR Congo, kisha nao kuamua kumuondoa rasmi katika timu ya taifa hilo.
Zahera alikuwa kocha msaidizi wa DR Congo akiteuliwa kumsaidia aliyekuwa kocha wa timu hiyo Muargentina Hector Cuper ambaye naye alishatimuliwa kutokana na matokeo mabovu.
Tayari DR Congo imeshapata kocha mpya ambaye ni Mfaransa Sebastian Desabre, huku wakibadilisha maisha ya makocha hao ambao awali walikuwa sio lazima waishi muda wote nchini humo.
Congo sasa wamewataka makocha wote kuhakikisha wanaishi nchini humo na kufuatilia kwa karibu wachezaji ambao wanacheza ligi ya kwao baada ya kuona mastaa wao wanaocheza Ulaya wanakosa uzalendo wakivaa jezi za taifa hilo.
Sharti hilo ndio limemng’oa Zahera ambaye ameshindwa kukubaliana na mabosi wake akitaka kuendelea kufanya kazi nje ya taifa hilo huku akija mara tu timu hiyo inapikuwa na mchezo.
DR Congo imeshampa ukocha Mhispania Raphael Cuadros akichukua nafasi ya Zahera huku pia kocha wa zamani wa TP Mazembe ,Pamphil Mihayo akiwa kocha wa tatu.
Zahera amelithibitishia Mwanaspoti juu ya uamuzi huo akisema ameamua kukataa maamuzi hayo kufuatia familia yake kumzuia kukaa nchini humo.
“Familia yangu nikiwaambia nakwenda Congo wanakosa amani wanafahamu ni nyumbani, lakini wanakuwa na wasiwasi juu ya usalama wangu.