Lugha 10 za Asili Zinazozungumzwa zaidi Afrika, Kiswahili Namba Moja


Orodha ya Lugha za Asili Zinazozungumzwa Zaidi barani Afrika, Kiswahili kinara.


1. KiSwahili ikipatikana hasa pwani ya Afrika mashariki (200 million)


2. Hausa inapatikana Afrika magharibi na Afrika ya kati (120 million)


3. Amharic inapatina Ethiopia (57 million)


4. Yoruba inapatina Afrika magharibi hasa mataifa ya Nigeria, Benin na Togo (50 million)


5. Igbo inapatikana nchini Nigeria (45 million)


6. Fulani inapatikana mataifa ya Nigeria, Niger, Guinea, Mali, Senegal, Cameroon na Ghana (41.6 million)


7. Oromo inapatikana baadhi ya ameneo ya Ethioa, Kenya, na Somalia (37.4 million)


8. Berber inapatikana Tunisia, Mali, Libya, Misri, Mauritani na Canary (32 million)


9. IsiZulu Inapatikana Afrika Kusini, Niger, Congo (28 million)


10. Malagasy inapatikana Madagascar (20M)


Lugha ya Kiswahili ni cha lazima kufundishwa kama somo katika Shule za Msingi na Sekondari nchini Uganda, Kenya na Tanzania ingawa taifa la DR Congo linapanga kuifanya lugha rasmi.


Mbali na hilo Lugha ya Kiswahili inafundishwa katika vyuo vikuu vya kigeni nchini Marekani, Italia, Uholanzi, Uingereza, Canada, Ujerumani na mataifa mengine.


Kiswahili kwa sas akinaelezwa kuwa kipo katika mtaala wa shule za msingi nchini Afrika Kusini.


Kiswahili pia kinazungumzwa nchini Somalia, Yemeni na Oman (Kusini).


Iliwahi kuzungumzwa na watu wa Antalaotra huko Madagaska Kaskazini Magharibi.


Ifahamike kuwa Kiswahili ni lugha rasmi ya taifa kama mataifa Tanzania ikiongoza mataifa mengine ni Kenya, Rwanda, Uganda, mbali na hilo Kiswahili kimepitishwa kutumika katika mikutano ya AU, na pia katika EAC (Jumuiya ya Afrika Mashariki.


Uganda ilifanya Kiswahili kuwa lugha rasmi Julai 5. Kilifanywa kuwa cha lazima katika shule za msingi na upili.


Ifahamike kuwa Kiswahili ni lugha ya kienyeji inayozungumzwa zaidi barani Afrika kwa mujibu wa tafiti za majarida mbalimbali hasa jarida la Africa Fact Zone zikionyesha kuwa Kiswahili ikiwa na wazungumzaji milioni 200 ikijumuisha nchi kama Tanzania, Kenya, Uganda, DR Congo, Komoro, Rwanda, Msumbiji, Malawi, Zambia, Burundi, India.


Kwa upande wa Tanzania inaogoza kuzungumzwa zaidi kwani inakadiriwa kuwa Watanzania zaidi ya milioni 50 wanazungumza lugha ya kiswahili ingawa kuna raia kutoka mataifa ya nje ambao hawazungumzi Kiswahili licha ya kupewa uraia.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad