Mabasi Mengi ya Shule ni Mabovu


Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Kipolisi Temeke limesema katika ukaguzi wa Mabasi ya Shule yanayobeba Wanafunzi wamebaini mengi yao yana ubovu wa mfumo wa breki na matairi na kuagiza Mabasi hayo yafanyiwe marekebisho.

Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Kipolisi Temeke SP. Africanus Sulle amesema hayo wakati akiongea na Madereva wa Mabasi hayo na Wamiliki wa Shule binafsi za Wilaya ya Kigamboni na kuwataka wawe wanayakagua mara kwa mara kuokoa maisha ya Wanafunzi.

"Magari mengi ya ubovu mkubwa kwasababu ni hatarishi wa mfumo wa breki lakini pia tumegundua ubovu mkubwa kwenye matairi, wengi wenu hamnunui matairi mapya, mnanunua matairi yaliyochongwa yanayopatikana chang'ombe mnakuja kubebea Watoto wetu”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad