Ofisi ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Masuala ya Afrika imesema jukumu jipya la Uhuru Kenyatta limekuja wakati mwafaka
Ofisi ilisema Uhuru atachukua jukumu muhimu katika kumaliza mzozo Kaskazini mwa Ethiopia na Mashariki mwa DRC
Rais William Ruto alimteua rais anayeondoka kuwa mjumbe wa amani wa Kenya katika eneo hilo
Ofisi ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani inayoshughulikia masuala ya Afrika imempongeza Rais William Ruto kwa kumteua rais mstaafu Uhuru Kenyatta kuwa mjumbe wa amani Kenya.
Marekani Yapongeza Hatua ya William Ruto Kumteua Uhuru Mjumbe wa Amani wa Kenya
William Ruto na Uhuru Kenyatta wakiwa Kasarani. Picha: William Ruto.
Katika taarifa yake mnamo Ijumaa, Septemba 16, Ofisi hiyo ilisema Uhuru ataendelea na jukumu muhimu katika kusukuma amani katika Pembe ya Afrika na eneo la Maziwa Makuu.
"Tunakaribisha kuteuliwa kwa Uhuru Kenyatta kuwa mjumbe wa amani kwa vita vya Kaskazini mwa Ethiopia na Mashariki mwa DRC. Wakati muhimu kwa migogoro yote miwili - kazi yake itakuwa muhimu."
Magazeti ya Kenya Ijumaa, Septemba 16: William Ruto ataka walioiteka nyara serikali ya Jubilee kuadhibiwa
Wakati wa utawala wake kama rais, Uhuru alichukua nafasi muhimu katika mazungumzo ya amani nchini Ethiopia, Sudan Kusini, DR Congo na Somalia.
Wakati wa hotuba yake ya kuapishwa, Rais Ruto alifichua kuwa Uhuru ataendelea kuwakilisha nchi kama mjumbe maalum kuhusu masuala ya amani ndani ya nchi jirani.
Katika hotuba yake, Ruto aliahidi kuendelea na mipango ya amani iliyokuwa ikiendelezwa na Uhuru.
"Kenya itaendelea kutekeleza jukumu lake katika diplomasia ya nchi mbili na kimataifa, ikithamini kwamba sisi ni wenyeji wa mashirika makubwa ya kimataifa, ikiwa ni pamoja na UN. Ninajitolea kwa mipango ya amani katika eneo letu, ikiwa ni pamoja na Ethiopia na kanda ya ziwa kuu," Ruto alisema
Ruto alidokeza kwamba alishirikiana na rais anayeondoka, na amekubali kuendelea kuwa mjumbe wa amani kwa niaba ya Kenya.