Marufuku kufunga biashara ili kufanya usafi: Chalamila



Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Albert Chalamila amepiga marufuku suala la Watumishi wa kata na mitaa kuwalazimisha wafanyabiashara kufunga maduka ili kufanya usafi, akisema hali hiyo halikubaliki na badala yake usafi ufanyike kila siku, bila kuathiri ufanyaji wa biashara.

Chalamila ameyasema hayo, wakati akizungumza na Shirikisho la Umoja wa Wamachinga, Mama Lishe/Baba Lishe, Jamii Mpya, Wanawake Wafanyabiashara, Jukwaa la Uwezeshaji wananchi kiuchumi na Shujaa wa Maendeleo wa Mkoa wa Kagera.


Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Albert Chalamila (wa tano kutoka kushoto), katika picha ya pamoja na baadhi wa Viongozi washiriki.
Amesema, dhana ya kuchagua siku moja kuwa ni siku ya usafi inarudisha nyuma ukuaji wa kiuchumi na kupelekea baadhi ya wafanyabiashara kutofungua biashara zao na hivyo kuingia hasara wao na Serikali kukosa mapato.

“Tunatakiwa kujiaandaa na mapokeo ya mabadiliko ya kifikra na kushirikiana katika kuzitumia fursa zilizopo ili kuinua uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kiujumla, dhana ya kuchagua siku moja kuwa ni siku ya usafi inarudisha nyuma ukuaji wa uchumi” amesema Chalamila.


Baadhi ya Wanashirikisho la Umoja wa Wamachinga, Mama Lishe/Baba Lishe, Jamii Mpya, Wanawake Wafanyabiashara, Jukwaa la Uwezeshaji wananchi kiuchumi na Shujaa wa Maendeleo wa Mkoa wa Kagera.
Aidha, amesema katika uongozi wake hatopenda kuona maelewano hafifu baina ya viongozi hasa mvutano wa matumizi ya fedha za utekelezaji wa miradi na kuwataka kuchangamkia fursa zilizopo kwa lengo la kupiga hatua za maendeleo, zilizo na maslahi kwa umma.

Awali, Katibu Tawala Mkoa, Toba Nguvila alieleza kuwa atasimamia kuhakikisha hakuna urasimu katika ofisi za Serikali wakati wa kuzifikia fursa mbalimbali, ikiwemo mikopo ya Vikundi vya akina mama, vijana na watu wenye ulemavu.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad