Mayay avunja ukimya juu ya hatima yake



SIKU chache tu baada ya kutambulishwa rasmi na kupewa baadhi ya majukumu ya kuanza nayo katika cheo kipya alichoteuliwa, Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo, Ally Mayay amevunja ukimya juu hatma yake ya uchambuzi wa soka huku akisisitiza mipango yake kama kiongozi.

Mayay aliteuliwa hivi karibuni na Waziri wa Sanaa, Utamaduni na Michezo, Mohammed Mchengerwa kuchukua nafasi ya Yusuph Singo aliyepangiwa majukumu mengine na juzi alitambulishwa rasmi wakati wa hafla ya kuiaga timu ya taifa ya wanawake ya U17, Serengeti Girls.

Akizungumza na Mwanaspoti, Mayay alisema; “Nilikuwa nafanya vile kwa mapenzi, ila kwa sasa huo muda hautakuwepo, kwa kuwa mazingira ya kusimamia kurugenzi yote ya michezo itanibana, labda ikiotokea ni mara mojamoja sana, lakini kwa sasa kwenye kuchambua nimetoka.”

Mayay aliwatoa hofu baadhi ya wadau wa michezo ambao walimuomba kutoegemea kwenye soka zaidi ambako walizoea kumuona huko ambapo mbali na kucheza kwa mafanikio, pia amekuwa kiongozi na kugombea nafasi kadhaa.


“Kurugenzi ya michezo inashughulika na michezo yote nchini, uzuri nafahamu thamani ya mkimbia, bondia, mcheza judo muogeleaji, na kila mchezaji kwa nafasi yake na kikubwa ni kwamba wanamichezo tuna zungumza lugha moja.

“Tutashauriana, kila mchezo una wataalamu wake, lakini wote ni familia moja, hivyo tutakuwa na maamuzi ya pamoja ambayo tunaamini yatatufikisha kwenye mafanikio,” alisema Mayay.

Kuhusu mipango yake, Mayay alisema majukumu ya serikali yapo kwenye mpango kazi, na katika kitengo chake amekuta mpango kazi wa miaka mitano ambao upo, jukumu lake na wadau wa sekta hiyo ni kuutekeleza huo mpango kazi. “Mpango kazi umejitosheleza, jukumu letu ni kuutekeleza tu, umegusa maeneo mbalimbali ikiwamo ya miundo mbinu.”


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad