Mkoani Njombe, linamshikilia Happiness Mkolwe (27) kwa tuhuma za mauaji ya mtoto Jackson Kiungo (6), mwanafunzi wa darasa la kwanza katika Shule ya Msingi Ihanga na kujaribu kumfukia katika shimo alilolichimba.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Hamisi Issah.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Hamisi Issah, alisema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari mkoani hapa.
Kamanda Issah, alisema siku ya tukio mwanafunzi huyo alikwenda saluni kunyoa lakini katika hali ambayo si ya kawaida, Mkolwe huyo alimfuata na baada ya kumaliza kunyolewa, alimchukua na kuondoka naye kwenda alikojua mwenyewe.
Alisema alipofika huko, alimsababishia kifo na kumvua nguo kisha kumfukia na baadaye kumfunika na mabanzi ambayo yalikuwapo katika eneo hilo.
Issah alisema, mwanamke huyo baada ya kufanya tukio, aliamua kuchimba kaburi ili amfukie.
"Lakini macho kuona walimwona mama huyo, hivyo hakuendelea na tukio hilo la kumfukia ingawa tayari alikuwa ameazima vifaa kwa ajili ya kutenda jambo hilo. Baada ya kufuatilia, tumeona vitu vya namna hiyo," alisema Issah.
Kamanda Issah alisema jambo la kushangaza, ni kuwa mwanamke huyo alipoulizwa alikataa katakata lakini baadaye alionyesha mpaka nguo ambazo mwanafunzi huyo alivaa kabla ya kukutwa na umauti.
Alisema kisa kilichosababisha mauaji hayo, kwa mujibu wa maelezo ya mwanamke huyo, ni kwamba wametengana na mumewe na kuna mwanamke mwingine ambaye ni mama wa mwanafunzi huyo alikuwa anakunywa pombe na mumewe, hivyo alipopewa taarifa hiyo na watu wake, aliamua kulipiza kisasi.
Issa alisema, mwanamke huyo alikamatwa juzi baada ya jeshi hilo kupata taarifa kuwa Septemba 6, mwaka huu, kuna mwanafunzi amepotea.
Alisema, ukatili dhidi ya watoto kwenye baadhi ya maeneo mkoani Njombe upo ndiyo maana mkoa huo umeelezwa kuwa ni moja ya maeneo yaliyokithiri matukio hayo.
"Ndiyo maana walikuwa wanasema watoto wameuawa na watu wasiojulikana kitu ambacho si kweli bali ni mambo ya kifamilia na mtu wa karibu wanayafanya mauaji hayo," alisema Issah.
Alisema, matukio yanayohusisha mauaji ya watoto wengi wao ni umri wa miaka sita kwani akivuka umri huo inakuwa bahati kwa mtoto huyo.