Kesi namba 12 inayomkabili Diana Bundala maarufu kama mfalme Zumaridi na wafuasi wake 84 ya kufanya mkusanyiko usio halali leo hii imeshindwa kuendelea baada ya mshtakiwa namba 38 aitwaye Maria Julius kuanguka ghafla mahakamani na kukimbizwa hospitali kwa ajili ya matibabu
Ikumbukwe kuwa hivi karibuni Diana Bundala maarufu kama mfalme Zumaridi aliwahi kuiomba mahakama kesi isiendelee ili aweze kupata matibabu kutokana na maeneo mbalimbali ya mwili wake kuuma, Zumaridi na wafuasi wake 84 walikamatwa tarehe 26 ya mwezi wa pili mwaka huu na wengi wao wanadai wapigwa na askari polisi wakati wa ukamataji
Baada ya mshtakiwa huyo namba 38 ajulikanaye ka jina la Maria Julius kuanguka mahakani Wakili upande wa utetetzi Amri Linus akaiomba mahakama Ushahidi usiendelee ili mshtakiwa huyo akapatiwe matibabu
Washtakiwa wote 85 katika kesi hii namba 12 ya mwaka 2022 wanatetewa na jopo la mawakili watatu akiwemo Steven Kitale, Amri Linus Pamoja na Erick Mutta nimezungumza na Erick Mutta nje ya mahakama
Mahakam ya hakimu mkazi mkoa wa Mwanzaikiongozwa na hakimu Clescensia Mushi ikaiahirisha kesi hiyo hadi hapo kesho kesi hiyo itakapoendelea.