Kuna nyakati Morrison anaweza kuamua mechi peke yake. Anajua kuwahadaa mabeki na kuwafanya anachojisikia.
Mfano namna alivyoangushwa dhidi ya Azam na kuipatia timu yake penalti waliyokosa. Akili kubwa sana.
Fundi mmoja wa mpira pale Yanga. Anajua sana soka huyu mwamba kutoka Ghana.
Ana uwezo mkubwa wa kumiliki mpira. Ana kasi na uwezo mkubwa wa kupiga chenga. Ni fundi kweli kweli.
Kuna nyakati Morrison anaweza kuamua mechi peke yake. Anajua kuwahadaa mabeki na kuwafanya anachojisikia. Mfano namna alivyoangushwa dhidi ya Azam na kuipatia timu yake penalti waliyokosa. Akili kubwa sana.
Hii ndiyo sababu Yanga imemsajili kwa mara ya pili. Haikushangaza sana. Ndani ya Uwanja, Morrison atakupa kile unachohitaji.
Tatizo moja la Morrison ni nidhamu yake. Ana matukio ya kushangaza sana. Ni kama hili alilomfanyia mchezaji wa Azam FC majuzi.
Alimkanyaga bila sababu ya msingi. Ilikuwa ni kadi nyekundu ya moja kwa moja.
Bahati mbaya mwamuzi hakuona lakini ni wazi Kamati zitamshughulikia.
Hii ndio changamoto ya Morrison. Pale Simba aliwahi kuvua nguo na kubaki na ile ya kufunika nyeti tu. Tena alivua kwenye mechi ambayo iko mbashara kwenye luninga.
Baadaye akafungiwa mechi tano kwa makosa ya kimaadili. Huyu ndio Morrison. Fundi wa mpira lakini kichwani mwake ni kama ana mdudu.
Siyo mtu wa kumwekea dhamana sana. Unaweza kumuweka kwenye mipango yako na akakuzingua. Anaweza kufanya jambo ambalo hujalitegemea hata kidogo.
Nje ya Uwanja anaweza kukukera pia. Simba waliwahi kukiri kuwa amekuwa na tabia ya kuondoka kambini mara kwa mara.
Tena bila kuaga. Kwa kifupi, Morrison akili zake anazijua mwenyewe.