Muuguzi Hospitali Amana kortini kwa ubakaji, ulawiti




Muuguzi Hospitali Amana kortini kwa ubakaji, ulawiti
MTUMISHI wa Hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam, Joseph Mwampola (59), amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa mashtaka ya ubakaji na ulawiti.

Mshtakiwa ambaye ni muuguzi katika hospitali hiyo, alifikishwa mahakamani hapo jana na kusomewa mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Yusto Luboroga.

Akisoma hati ya mashtaka, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Sylvia Mitanto, alidai mshtakiwa huyo alitenda makosa hayo katika maeneo mawili tofauti.

Ilidaiwa kuwa shtaka la kwanza la ubakaji mshtakiwa huyo katika tarehe isiyojulikana ndani ya hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam, alimbaka binti wa miaka 17.


Katika shtaka la pili la ubakaji Mwampola alidaiwa kumbaka binti huyo, kosa ambalo alilitenda Mei 31, 2022, katika nyumba ya kulala wageni iliyotajwa kwa jina la Pazuri Lodge.

Iliendelea kudaiwa kuwa shtaka la tatu ni la kulawiti ambapo katika tarehe isiyojulikana katika hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam, alimlawiti binti huyo akijua wazi jambo hilo ni kinyume na sheria.

Mshtakiwa alikana shtaka. Wakili Mitanto alidai upelelezi umekamilika na aliomba mahakama ipange tarehe ya kumsomea mshtakiwa maelezo ya awali.


Kesi hiyo iliahirishwa hadi Oktoba 5, 2022 na mshtakiwa yuko nje baada ya kutimiza masharti ya dhamana ya kuweka bondi ya Sh milioni tano na kupeleka wadhamini wawili wenye utambulisho, walioweka bondi ya Sh milioni tano kila mmoja.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad