Mwamnyeto, Mkude, Shomari,Tshabalala Watemwa Stars




Kocha mkuu wa timu ya taifa ‘Taifa Stars’, Hanoor Janza ametaja kikosi cha wachezaji 23 kitakachoingia kambini kwa ajili ya kujiandaa na mechi za kirafiki zilizopo kwenye kalenda ya FIFA akiwatema Bakari Mwamnyeto na Mohamed Hussein ‘Tshabalala’.
Kocha mkuu wa timu ya taifa ‘Taifa Stars’, Hanoor Janza ametaja kikosi cha wachezaji 23 kitakachoingia kambini kwa ajili ya kujiandaa na mechi za kirafiki zilizopo kwenye kalenda ya FIFA akiwatema Bakari Mwamnyeto na Mohamed Hussein ‘Tshabalala’.
Janza pia amemrejesha kikosini beki Abdi Banda anayecheza soka la kulipwa katika klabu ya Chipa United ya Afrika kusini akiongeza nguvu katika kikosi kitakachocheza mechi za kirafiki zilizopo kwenye kalenda ya FIFA.

Banda mara ya mwisho kuitwa kwenye timu ya taifa ni kipindi alichokuwa anacheza soka la kulipwa katika klabu ya Baroka ambayo baadae aliachana nayo na kurejea nchini msimu uliopita na kucheza Ligi Kuu akiwa na Mtibwa Sugar.

Ingizo la Abdi Banda kwenye kikosi kunamuondoa nahodha wa Yanga, Bakari Mwamnyeto wakati huo huo David Luhende ameingia akichukua nafasi ya Mohamed Hussein ‘Tshabalala’.

Wachezaji wengine walioachwa kwenye kikosi hicho ni Shomari Kapombe, George Mpole, Reliants Lusajo, John Bocco, Farid Mussa, Kibu Denis na Jonas Mkude.


Na nafasi zao zimechukuliwa na Datius Peter (Kagera Sugar) Abdalah Mfuko (Kagera Sugar) Carlos Protas (Tusker Fc), David Ulomi (Moroka Swallows) na Said Hamis (Hatta Club)

Akizungumzia upande wa kuita sura mpya nyingi, Janza amesema imetokana na viwango ambavyo wamevionyesha kwenye timu zao.

“Sisi benchi letu ni kuangalia kila mchezaji ambaye anafanya vizuri na tunamuita kwa ajili ya kuipambania timu ya Taifa, milango bado ipo wazi kwa wachezaji wengine.” amesema Janza.


Upande wa kocha msaidizi, Mecky Maxime akizungumzia upande wa kukosekana mchezaji Tepsi Evance amesema , ”Sio yeye tu hata Sopu (Abdul Suleiman) tumewaweka kwenye timu chini ya miaka 23 kwa sababu wana mashindano yao.”

Stars inatarajia kuanza kuingia kambini Jumamosi na Jumatatu watafanya mazoezi mepesi kisha Jumanne wataondoka kwenda nchini Libya kucheza mechi za kirafiki mbili na timu hiyo kuanzia tarehe 20.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad