Mwaka 1915, mwanamke mmoja alichelewa kwenye maziko ya Dada yake. Pindi alipofika, aliomba Jeneza la Dada yake huyo lifukuliwe na lifunuliwe ili kusudi amuone kwa mara ya mwisho. Wakati anafika Jeneza lilikuwa tayari limeshushwa chini na udongo kiasi umeanza kutupiwa.
Baada ya Jeneza kufunuliwa, Dada yake huyo aitwaye (Essie Dunbar) aliamka na kukaa akiwa ndani ya Jeneza na kisha kumpa tabasamu la nguvu mdogo wake. Essie aliyekuwa na umri wa miaka 30 wakati ‘anafariki’ alienda kuishi tena kwa miaka 47.
Dr. Briggs toka South Carolina ni daktari ambaye alishughulikia mwili wa Essie Dunbar, alisema alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa ‘Epilepsy’ ambao ni kima Kifafa, hivyo hufanya Seli za kwenye ubongo kushindwa kufanya kazi. Hivyo alimtangaza kuwa ‘amefariki’ kutokana na kutoonekana dalili zozote za uhai kwani alikuwa hapumui wala kutingishika.