Mwanamke Aua Mtoto wa Mchepuko wa MUME Wake, Akutwa Akimchimbia Kaburi Amzike

 


Polisi Mkoani Njombe wanamshikilia Happiness Mkolwe (27) Mkazi wa Ihanga Halmashauri ya Mji wa Njombe kwa tuhuma za kumuua Jackson Kihungo (6) Mtoto wa Shule ya Msingi Ihanga anayedaiwa kuwa ni Mtoto wa Mwanamke anayehusishwa kuwa na mahusiano na Mume wake (Mchepuko wa Mumewe).


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe Hamis Issah amesema Mwanamke huyo alimchukua Mtoto alipokuwa akitoka salumi na kumsababishia kifo na kumfukia kwenye takataka za mbao kabla ya kushtukiwa alipokuwa akichimba shimo kwa ajili ya kumfukia.


“Alivyomsababishia kifo alimvua nguo na kumpeleka kwenye takataka za mbao alikochimba na kumfukia kwasababu ni laini lakini haikutosha aliamua kuchimba kaburi pembeni ili amfukie, Mama huyu alishindwa kuendelea kwakuwa Watu waliona”


Kamanda Issah amesema sababu ya Mwanamke huyo kutekeleza mauaji hayo ni wivu wa mapenzi kutokana na kupewa taarifa kuwa Mume wake aliyetengana nae kwa muda anakunywa pombe na Mwanamke mwingine.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad