Raia wa Uganda, ‘Nabii’ Kintu Dennis amekamatwa na Polisi na kisha kufunguliwa mashtaka ya kushambulia na kusafirisha watu, baada ya kusambaa kwa video moja mtandaoni ikimuonesha akiwachapa viboko waumini wa kanisa lake.
Dennis (42), ambaye ni mkazi wa Hoima akisadikika kuwa ni kiongozi wa Kanisa la ‘Empowerment Church International, alikamatwa na Polisi siku ya Jumatano Septemba mosi, 2022 pamoja na waumini wake wanne kufuatia malalamiko kuhusu video hiyo.
Picha tofauti za Kintu Dennis (42), aliyekamatwa na Polisi wa Uganda kwa kuchapa waumini. Picha na Tuko.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi, imesema Dennis aliwaamuru viongozi wa kanisa kwenda madhabahuni na kuwachapa viboko waumini akiwataka kuacha kuhudhuria maombi na kupoteza fursa ya kushika kipaza sauti chake.
Hata hivyo, katika mahojiano Nabii huyo alisema alikuwa akifanya onesho la jinsi Yesu alivyowatendea wale aliowakuta wakiuza bidhaa kanisani, na kwamba ujumbe wake umepokelewa tofauti na jamii.