Nyota wa Kimataifa wa Ufaransa Kylian Mbappe Yupo Upande wa Pogba, Tuhuma za Uchawi

Nyota wa Kimataifa wa Ufaransa Kylian Mbappe anayekipiga katika klabu ya Psg ameamua kuvunja ukimya na kulizungumzia sakata la mchezaji mwenzake wa timu ya taifa ya Ufaransa Paul Pogba.





Mbappe amesema kuwa anaamini kile kilichozungumzwa na Pogba, na kuwa maneno yake ni ya kweli dhidi ya yale yaliyozungumzwa na kaka yake Pogba.


Mbappe ameeleza hayo akijibu swali la mwandishi wa habari usiku wa Jana kwenye Press kuelekea mtanange wao (PSG vs Juventus) wa Ligi ya Mabingwa Ulaya leo usiku.


Itakumbukwa, wiki iliyopita Paul Pogba alijikuta kwenye shutuma nzito kwa kile kilichotokea kati yake na familia yake. Pia katika kitu ambacho kiliwashangaza wengi ni pale Pogba alipokiri kuwa ni kweli hutumia mganga wa jadi kumpatia dawa ili ajikinge na kupata majeraha ya uwanjani.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad