‘Panya road’ 135 wakamatwa, vituo vya polisi sasa saa 24




Dar es Salaam. Jumla ya wahalifu 135 wamekamatwa ndani ya siku nne jijini Dar es Salaam tangu kuanza kwa operesheni ya kuzia uhalifu iliyoanza Septemba 15, 2022.

 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam (RC), Amos Makala amesema wengi waliokamatwa vijana wenye umri kati ya miaka 14 na 30 waliobainika kuhusika na matukio ya uvamizi mitaani maarufu kama Panya Road.

Makala amesema baada ya kuwakamata vijana hao walipohojiwa ilibainika viongozi wa magenge hayo baadhi yao waliwahi kutumikia vifungo mbalimbali magerezani.

“Nilitangaza Septemba 15 kuwa tumeongeza askari 300 lakini watu hawa hawakutaka kusikia wakaenda kujaribu kule Makongo na Ubungo.


Katika siku hizi nne, tumeweza kukamata vitu mbalimbali vya wizi vikiwemo runinga 23 na watuhumiwa 135 wamekamatwa wanaendelea na mahojiano.

“Wamekamatwa pia wanunuzi wakubwa watano wa bidhaa za wizi,” amesema Makala”

Mkuu huyo wa mkoa amesema kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa imekutana na kuweka mkakati kuanzia sasa vituo vyote vya polisi vitafanya kazi kwa saa 24.

“Vile vituo vilivyokuwa vinafungwa saa 12, sasa vitafanya kazi saa 24 hii ina maana polisi hawatolala na wako tayari kushirikiana na wananchi,” amesema Makalla na kuongeza:

“Kila kata itakuwa na gari kwa ajili ya doria, ulinzi utazidi kuimarishwa na tumekubaliana kila mtaa kuwa na mkutano wa wiki ya kwanza ya mwezi kujadili suala la ulinzi na usalama,” amesema Makala.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad