Aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Tanzania (CAG), Profesa Mussa Assad amesema anaamini suala la #Tozo lina hasara kubwa kuliko faida kwa Serikali
Amesema "Kuna namna nyingine ya kupata fedha, mfano Viongozi wanaotumia magari ya Serikali yenye gharama kubwa kwa shughuli za kiofisini na binafsi, hao ndio wanatakiwa kulipa kodi kwa kuwa wanapata faida ambazo si za kifedha"
Pia, ametoa mfano wa wanaotakiwa kukatwa kodi kuwa ni Mawaziri, Makatibu Wakuu, Wakurugenzi, Wakuu wa Mashirika ya Umma huku akisema kama Viongozi hao wananunua magari yawe ya gharama ya chini kidogo ili nafuu iwe kwa Wananchi