Rais Samia Akutana na Ruto Kabla ya Kuapishwa



Nairobi. Rais mteule wa Kenya, William Ruto amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ofisini kwake, Karen, jijini Nairobi nchini Kenya.

Ruto amekutana na Rais Samia saa chache kabla ya kwenda kuapishwa kuwa Rais wa Taifa hilo kuchukua nafasi ya Uhuru Kenyatta anayemaliza muda wake wa uongozi wa miaka kumi.

Rais huyo mteule ameweka picha kwenye ukurasa wake wa Twitter zikionyesha wakiwa kwenye mazungumzo huku akiandika kuwa mwenyeji wa Rais Samia ofisini kwake Karen jijini Nairobi nchini Kenya.

Rais mteule wa Kenya, William Ruto akiwa na Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ofisini kwake, Karen, jijini Nairobi nchini Kenya


Rais Samia ambaye aliwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta, Nairobi mapema leo atakuwa miongoni mwa wakuu wa nchi na wageni mbalimbali watakaoshuhudia Ruto akiapishwa kuwa Rais wa Kenya leo Jumanne, Septemba 13, 2022 katika Uwanja wa Kasarani.

Taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu iliyotolewa jana Jumatatu ilisema, Rais Samia anaambatana na viongozi mbalimbali wakiwemo mawaziri wa Tanzania na Zanzibar, akiwemo Balozi Libarata Mulamula, Waziri wa Mambo ya Nje.

Ruto ambaye ni Naibu wa Rais, ataanza safari ya kuwaongoza Wakenya, baada ya kuibuka mshindi katika uchaguzi mkuu uliofanyika Agosti 9, 2022 kwa kumshindi hasimu wake wa karibu, Raila Odinga mwenye miaka 77.


Sherehe hiyo ya uapisho inatarajiwa kuhudhuriwa na Marais 20 kutoka Afrika wakiwamo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad