Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesikitishwa na kifo cha Malikia Elizaberth II wa nchini Uingereza, kilichotokea jana Alhamisi Septemba 8, 2022 katika visiwa vya Balmoral nchini Scotland alipokuwa anapatiwa matibabu.
Katika ukurasa wake wa Twitter, Rais Samia ameandika, “Nimesikitishwa na taarifa za kifo cha Malkia Elizabeth II. Kwa niaba ya Watanzania wote, natuma salamu za pole kwa familia ya [email protected] na raia wote wa Uingereza. Malkia atakumbukwa duniani kote kama nguzo ya Amani, Umoja na Utulivu.”
Nimesikitishwa na taarifa za kifo cha Malkia Elizabeth II. Kwa niaba ya Watanzania wote, natuma salamu za pole kwa Familia ya Kifalme @RoyalFamily na raia wote wa Uingereza. Malkia atakumbukwa duniani kote kama nguzo ya Amani, Umoja na Utulivu. pic.twitter.com/XsIpsYtG94
— Samia Suluhu (@SuluhuSamia) September 8, 2022
Elizaberth II aliezaliwa jijini London April 21, 1926, aliukwa wadhifa wa Malkia akiwa na umri wa miaka 25, mnamo mwaka 1952 baada cha kifo cha baba yake aliyekuwa mfalme wa taifa wa taifa hilo David IV.
Malkia Elizaberth II amefarikii akiwa na umri wa miaka 96, lakini wengi watamkumbuka kwa yale mazuri aliyoyafanya na lile la kuweka rekodi ya kuwa mtawala wa kifalme aliyeongoza kwa muda mrefu mnamo Septemba 9, 2015, na kupita rekodi ya bibi wa bibi yake Malkia Victoria.