Sauti ya Mwanamuziki The Weeknd Yarudi Atangaza Kuendelea na Tour Baada ya Sauti Kukwama Akiwa Jukwaani

Mwimbaji wa muziki toka Canada, The Weeknd kupitia ukurasa wake wa Twitter, ameeleza kwamba sauti yake sasa iko poa na Daktari wake amemwambia anaweza kuendelea na tour yake "The After Hours Till Dawn Tour" kama kawaida.


Itakumbukwa, mwishoni mwa wikiendi iliyoisha mwimbaji huyo alilazimika kusitisha show yake ndani ya Uwanja wa SoFi huko California nchini Marekani baada ya sauti yake kugoma jukwaani wakati akiwa anatumbuiza.


Mkali huyo ambaye jin
a lake halisi ni Abel Tesfaye, kwenye show yake hiyo alikuwa katikati ya wimbo wake wa pili, "Cant feel my face" alipopoteza sauti. Hata hivyo, alisimamisha show na kuomba msamaha kwa mashabiki.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad