Seikali yamaliza utata wa madai ya trilioni 360




Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba ametoa ufafanuzi kuhusu wapi zipo shilingi trilioni 360 zilizopo kwenye mashauri ya madai 1,095.

Waziri Nchemba amesema, kuna jumla ya mashauri 400 katika mabaraza ya rufani za kodi (TRAT) yenye thamani ya shilingi trilioni 4.2 na dola za Marekani milioni 3.04 zinaendelea katika mabaraza hayo.

Hata hivyo Dkt. Nchemba amesema, serikali ilikubali kupokea shilingi bilioni 700 kutoka Barrick baada ya makubaliano baina ya timu ya serikali iliyoundwa na Rais wa serikali ya awamu ya tano Hayati Dkt. John Magufuli kufikia makubaliano ya pande zote na Barrick kuhusiana na madai ya shilingi trilioni 360.


Amesema baada ya makubaliano hayo ndipo ikaundwa kampuni ya Twiga ambayo inamiliki hisa asilimia 16 na Barrick inamiliki asilimia 84 ya kampuni hiyo.


Ufafanuzi huo wa waziri wa Fedha na Mipango unatokana na maswali ya Mbunge wa jimbo la Kisesa, Luhaga Mpina aliyetaka kufahamu kwa nini serikali imekubali kulipwa shilingi bilioni 700 kutoka kampuni ya Barrick badala ya shilingi trilioni 360 za awali.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad