Serikali Kuwashughulikia Wanaohamasisha Ushoga




Serikali imetangaza kuanza kuchukua hatua kali kwa watu watakaobainika kusambaza maudhui yanayohamasisha mapenzi ya jinsi moja.

Pia, amewatahadharisha viongozi wa makundi ya ya WhatsApp ma ‘admin’ ambao hawatafuata au kuchukua hatua kwa wanaosambaza maudhui ya mapenzi ya jinsi moja yakiambatanishwa na video au picha kuwa watachukuliwa hatua kali pamoja na vyombo vya habari.

Hayo yamesemwa leo Jumapili Septemba 11, 2022 na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye jijini Dar es Salaam.

Amesema hatua hiyo imekuja kufuatia kukithiri kwa vipande vya video zinazosambaa mitandaoni zikionyesha vitendo vya aina hiyo.


Waziri Nape amesema kuanzia sasa Serikali haitavumilia kuendelea kusambaa kwa maudhui hayo na itafanya hivyo kwa wote wanaosambaza hata kama wanafanya hivyo kwa lengo la kutahadharisha.

“Tumeendelea kufuatilia anga la mtandao wetu, liko salama isipokuwa hizi changamoto ndogo ndogo na hivi karibuni tunaona kumekuwa na usambaaji wa video zinazohamasisha ushoga na usagaji.

“Tumefuatilia kwenye vyombo vyetu ambavyo tumevipa leseni hakuna ambacho kinahusika katika hili, watu wanapakua kupitia pay tv matokeo yake zinasambaa kupitia mitandao ya kijamii hasa makundi ya WhatsApp,”amesema Nape na kuongeza.


“Sasa nitoe tahadhari tutakapoanza kuwazoa, hatutegemei taharuki maana hadi mimi kujitokeza kuzungumzia hili suala ni wazi kwamba tumeamua kulifanyia kazi. Kuweni makini huko kwenye mitandao na makundi ya WhatsApp hasa ma admin hatuna utani katika hili,” amesema .

Chanzo: Mwananchi
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad