Shaffih Dauda Ashindwa Kuelewa Kilichotokea Pambano la Mwakinyo, Haya Ndio Maswali yake Konki


Nina maswali yangu kadhaa tu, nimemsikiliza Kijana wetu na kutazama pambano ila kwenye kona yake hapakuwa na Kocha wake na waliopo walikuwa hawaelewi cha kumshauri Hassan.

Alionesha ameumia mguu wa kulia, mguu ni kiungo muhimu mno kwenye ring sasa kwanini hakushauri kutoka kwenye kamba? Muda mwingi alikuwa kwenye kamba.

Kijana wetu amepoteza pambano ila kuna sintofahamu nyingi sana, haswa ukizingatia uwezo mkubwa wa Hassan na namna alivyoanza fight na lilivyoisha.


Hassan ametuomba Watanzania msamaha, Hassan amelia kuonesha kiu yake ya kutaka kurejea na ushindi nyumbani ila kwasasa sisi bado tunawaza alipotezaje? Panaumiza sana kichwa haswa kwa uwezo mzuri wa Hassan.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad