Sintofahamu Baada ya Nyota wa Juventus Paul Pogba Kukiri Kutumia Uchawi



Mchezaji nyota wa Juventus Paul Pogba amekiri kwamba amekuwa akitumia uchawi lakini sio kwa kumroga mchezaji mwenzake wa Ufaransa Kylian Mbappé
Mvamizi huyo wa kimataifa wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 29, aliwaambia maafisa wapelelezi kwamba aliamua kutafuta huduma ya mganga kwa sababu za kibinadamu tu
Kwa mujibu wa ripoti, Paul Pogba amebadilisha nambari yake ya simu mara mbili tangu kuanza kwa kesi hiyo, ili kuepuka jaribio la ulaghai ambao alikuwa mwathiriwa
Paul Pogba amekiri kutumia uchawi katika mahojiano yake ya pili na maafisa wapelelezi wa Ufaransa.

Paul Pogba amekiri kwamba amekuwa akitumia uchawi lakini sio kwa kumroga mchezaji mwenzake wa Ufaransa Kylian Mbappé
Paul Pogba amekiri kwamba amekuwa akitumia uchawi lakini sio kwa kumroga mchezaji mwenzake wa Ufaransa Kylian Mbappé. Picha:@juventusfc Yanick Folly/ Getty Images @FFF.
Mathias Pogba, kaka mkubwa wa Paul alikuwa amefunguka mazito kumhusu mshindi huyo wa Kombe la Dunia mwaka wa 2018, akisema amekuwa akijihusisha na ushirikina na pia kumroga mwenzake wa Ufaransa Kylian Mbappé.

Lakini Paul Pogba amekiri kwamba amekuwa akitumia uchawi kwa sababu za kibinadamu wala sio kwa kumroga Mbappé

William Ruto Amlima Uhuru, Ampa Mkono Raila Odinga Kufuatia Uamuzi wa Korti
Kwa mujibu wa France Info, Paul aliwafichulia wapelelezi hayo wakati wa alipokuwa akihojiwa tena kwa mara ya pili, akidai kuwa ana ushahidi wa kuthibitisha.

Kiungo huyo wa zamani wa Man United, alidai kwamba alikuwa mwathiriwa wa jaribio la ulaghai ambalo kulingana naye lilipangwa na baadhi ya jamaa zake akiwemo kaka yake mkubwa Mathias Pogba.

Paul anaendelea kudai kuwa ni mwathiriwa wa jaribio la ulaghai wa pauni 13 milioni na kaka yake Mathias, na marafiki zake wa utotoni ndiyo waliopanga genge hilo.

Mathias aliwasha moto mtandao wa kijamii na video yake ya dakika tatu siku ya Jumapili, Agosti 28, akiahidi kuchapisha "ufichuzi mkubwa" kuhusu nyota huyo wa zamani wa Manchester United.

Paul hata hivyo, kwa majibu yake ya haraka kupitia kwa mawakili wake alidai kuwa kaka yake ni mmoja wa genge la uhalifu lililopangwa kumlaghai kitita cha Pauni milioni 13.

Mahat Somane: Wakili Mchanga wa IEBC Aonekana Kutamba Mahakamani
Lakini katika kuongezea chumvi kwenye jeraha, kaka mkubwa wa Pogba alifichua kuwa mdogo wake amekuwa akitumia mamilioni ya pesa katika uchawi ili kujilinda dhidi ya kupata jeraha.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad