Sintofahamu Kifo cha Mama na Mtoto: Wauguzi Watatu Washikiliwa na Polisi

 


Kutokana na mfululizo wa mikasa ya vifo vya uzazi, Senegal imewakamata wafanyakazi watatu wa afya baada ya kutokea kisa kipya cha kifo cha mama mjamzito na mtoto wake mchanga.


Katika mji wa kusini mashariki mwa eneo la Kedougou majira ya usiku, mwanamke na mtoto wake walifariki, na ripoti za vyombo vya habari vya ndani zimeelezea hali mbaya katika kituo cha afya cha Kedougou, takriban kilomita 700 kutoka mji mkuu wa Dakar nchini Senegal.


Watu hao watatu, akiwemo Daktari wa magonjwa ya wanawake, Daktari wa ganzi na muuguzi walikamatwa tangu Jumatano Agosti 31, 2022 na wanazuiliwa katika kituo acha gendarmerie ya Kedougou kwa kosa uzembe kazini.


Watoto Mil. 244 wakosa haki ya masomo


Hospitali ya Mame Abdoul Aziz Sy Dabakh, ambapo watoto 11 waliozaliwa walikufa kwa moto kufuatia hitilafu ya umeme, huko Tivaouane, Mei 26, 2022. – Picha na SEYLLOU / AFP.

Waliotengana na familia ‘wafunguka’ mazito

Mfumo wa huduma ya afya usio na ufadhili wa kutosha wa Senegal, unakabiliwa na uhaba wa wafanyakazi, vifaa na madawa, na taarifa hiyo ilisema upya wake hauna msaada kwa wafanyakazi ambao wanafanya kazi (mamia) ya kilomita kutoka jijini Dakar na wanakabiliwa na mazingira magumu ya kazi.


Kulingana na data za mwaka 2017, mfuko wa watoto wa UN unasema nchi hiyo ya Afrika Magharibi, ina kiwango cha vifo vya uzazi cha takriban watu 315 kwa kila watoto 100,000 wanaozaliwa, ikiwa ni juu ya wastani wa kimataifa wa vifo 211.


Chama cha Madaktari wa Wanawake na Madaktari wa Uzazi cha Senegal (ASGO), kimesema kati wafanyikazi watatu wa afya waliozuiliwa, mmoja ni mwanachama wake na kilitetea kuwa kukamatwa kwa wauguzi hao ni makosa.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad