Takribani Nyangumi 230 Wamekwama Ufukweni Mwa Bahari



Kiasi nyangumi 230 wamekwama magharibi mwa fukwe za kisiwa cha Tasmania ikiwa ni siku chache tangu nyangumi wengine 14 kupatikana wamekufa kaskazini mashariki mwa pwani ya kisiwa hicho.

Nusu ya Nyangumi wa kundi hilo jipya inaaminika bado wako hai na juhudi za kuwanusuru zinaandaliwa.

Haijafahamika mara moja sababu kamili ya Nyangumi hao kuogelea hadi fukwe zenye kina kifupi cha maji.

Hata hivyo mtaalamu mmoja wa ikolojia ya bahari wa chuo kikuu cha Griffith nchini Australia amesema huenda mabadiliko ya hali ya hewa yamebadili mkondo wa upatikanaji wa chakula kwa viumbe hao wakubwa kabisa duniani.

Matukio ya Nyangumi kukwama kwenye fuo za bahari yameongezeka miongo ya karibuni. Miaka miwili iliyopita Nyangumi wasiopungua 470 walinasa kwenye fukwe za kisiwa cha Tasmania na 111 pekee ndiyo waliokolewa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad