Mlima Kilimanjaro
TANZANIA imetajwa kuwa nchi ya nne kwa uzuri duniani na ya kwanza kwa Bara la Afrika kwa mujibu wa utafiti uliochapishwa na tovuti ya money.co.uk kutokana uzuri wa asili wa Taifa hilo lenye vivutio vya aina yake.
Tanzania ambayo inatajwa kuwa nchi nzuri kwa kutalii imepata alama 6.98 kati ya alama 10 zilizotumika kupima uzuri wa nchi huku ikiongoza kwa kuingiza fedha nyingi za kigeni kutokana na utalii kwa kukusanya dola bilioni 2.6 kwa mwaka 2019 na kutembelewa na watalii milioni 1.5.
Kilele cha Mlima Kilimanjaro
Licha ya janga la Corona lililovuruga shughuli za Kiuchumi duniani kote, ikiwemo watu kuzuiwa kusafiri kutoka nchi moja kwenda nyingine, uchumi wake wa kitalii uliporomoka na kufikia makusanyo ya dola milioni 795.8 mpaka Mei 2021.
Uzuri wa Mlima Kilimanjaro, mbuga ya wanyama ya Serengeti zinazoongoza Afrika ambayo imeshinda tuzo za hifadhi za Taifa ‘World Travel Awards’.
Watalii wakipanda Mlima Kilimanjaro
Ripoti hiyo inaonesha Indonesia ndiyo nchi nzuri namba moja duniani kwa kupata pointi 7.77 ikifuatiwa na New Zealand (7.27) na Colombia (7.16).
Orodha ya Nchi 10 nzuri zaidi Duniani
Indonesia
New Zealand
Colombia
Tanzania
Mexico
Kenya
India
France
Papua New Guinea
Comoros