Chelsea na Barcelona wamefikia makubaliano ya kumnunua Pierre-Emerick Aubameyang na mshambuliaji huyo mchana wa leo anaelekea jijini London baada ya mazungumzo ya siku ya mwisho kuhusu uhamisho wa pauni milioni 12 ambao pia unamjumuisha Marcos Alonso.
Aubameyang amekubali masharti ya mkataba wa awali wa miaka miwili na sasa anajiandaa kutua London ili kukamilisha uhamisho wake kabla ya muda wa mwisho wa dirisha la usajili halijafungwa.
Inadaiwa kuwa Klabu hya Chelsea imekodisha ndege ya binafsi ili kumfuata mshambuliaji huyo nchini Hispania na kumleta London, huku ndege hiyo ikitarajiwa kuondoka Barcelona majira ya saa saa 2:15 usiku.