Tumalize Ubishi Hapa Hapa, Nani zaidi Kwenye Mahaba, Wembamba vs Vibonge?


Rafiki, ngoja tuchangamshe kijiwe kidogo, mambo ya ushauri wa mapenzi nitaendelea nayo wiki ijayo, lakini leo hebu tujikite kwenya mjadala huu mzito.


Kwako wewe yupi bora? Mwembamba? Kipotabo? Kimbaumbau? Au kibonge? Minyamanyama? Au mirindimo?


Jamaa zangu wananinong’oneza kwamba wembamba ni moto wa kuotea mbali. Lakini nilipowauliza wataalam mbalimbali juu ya hilo, mambo yalikuwa ni moto!


Jibu nililopata ni kwamba kwa asilimia kubwa kuna ukweli; kwamba walio na wembamba wana uwezo wa kukimbia masafa marefu zaidi ya wale ambao ni wanene.


Japokuwa wanaweza kujitetea; lakini ukweli ni kwamba siyo wanene wengi wenye uwezo wa kukimbia masafa marefu.


Suala la mahaba linahitaji kutumia akili zaidi ya kufikiri kwamba utamridhisha mwenzi wako kwa sababu wewe ni mwembamba au mnene.


Ni wanawake wa aina gani wanavutia zaidi katika suala la mahaba? Utafiti unaonesha kuwa walio wembamba wana raha yake kwa sababu furaha ya wanaume wengi ni kudumu kwenye mapenzi kwa muda mrefu. Kwa hiyo walio wembamba wengi huwa hawachoki kwa haraka; miili yao haina mafuta mengi ya kuwachosha.


Walio wembamba wanaweza kukuruka huku na kule, wakati kwa wanene, kuna baadhi ya mambo hawawezi kwa sababu ya namna walivyo. Japo wapo wanene, na wana uwezo wa kwenda huku na kule, siyo wengi, kama walivyo watu wembamba.


Ni vigumu kuandika kwa kina, lakini kuna baadhi ya miondoko, watu wanene hawawezi. Kauli kama nimechoka huwa ni nyingi ukilinganisha na walivyo watu wembamba.


Hata hivyo, ninapozungumzia watu wanene, nazungumzia wale ambao hata kutembea kwao ni shida. Kwamba wana unene wa kupitiliza. Kitaalam huwa inashauriwa kuwa na minyamanyama, godoro linalobonyea huwa ni zuri kuliko lile ambalo gumu sana…si ndiyo jamani?


Mwanamke kwa mwanaume, unapaswa usiwe mkavu sana, maana kama ukiwa mkavu sana inasababisha maumivu, maana unaguswa na mifupa hadi inatia maumivu badala ya raha.


Ninachotaka kusema ni kwamba wanandoa wanapaswa kuhakikisha wanakula na kuondoa msongo wa mawazo ili wawe na miili inayonawiri…. Kuwa na mwenzi ambaye mwili umebaki mifupa…Mhh mnakuwa mnasababishiana maumivu jamani!


Wanawake walio wengi ambao ni wembamba ni watalam wa mapenzi kuzidi wanawake wanene, hii inatokana na tafiti mbalimbali zilizofanya na watalam wa masuala ya mapenzi kama Leticia Jackson wa Marekani, Profesa Benjamin James wa Ufaransa na Dk Edward Hulow wa Uingereza.


Wataalam hawa katika tafiti zao walizofanya katika nchi mbalimbali zinaonesha kuwa asilimia 85 ya wanawake wembamba wanajua miundo mingi wakati wa chakula cha usiku.


Hawa walio wengi, kabla ya kukutana nao inabidi ule ugali mbogamboga na nyama kavu…ukila chipsi kavu unaweza kujikuta unaanza kudanganya aaah unajua kazini kuna kitu nimesahau….aaah nahisi kiuno kinauma na utetezi mwingine wa sampuli hiyo.


Utafiti unaonesha asilimia 15 ya wanawake wanene ndiyo wanaojua kushiriki vizuri kwenye mapenzi. Sababu inayofanya wanawake wembamba kuwa wataalam sana ni kutoka na wepesi walionao.


Ni kutokana na wepesi wao, wanaweza kujikunja na kukaa namna yoyote. Japo siyo kila mwanamke anaweza kufanya hivyo kwenye mapenzi, wengine hawataki hata kutoa ushikiano katika mapenzi. Kuna wengine ni wembamba, lakini ni mizigo, kila anachoambia adai hawezi.


Kama mpenzi wako anafanya hivyo na huipendi tabia hiyo ni bora umwambie au umfundishe, kwa sababu siyo kila mtu anajua kila kitu japokuwa kila mwanaume ana uchaguzi wake ila uchaguzi wako isiwe sababu ya kuwanyanyapaa wanawake ambao siyo chaguo lako.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad