Ubalozi wataka maelezo Mtanzania aliyepigwa China



UBALOZI wa Tanzania nchini China, umeitaka serikali ya mji wa Xian kutoa maelezo juu ya tukio lililotokea jana Septemba 12, 2022, likimuhusisha raia wa Tanzania akishambuliwa na mwanamke raia China mjini humo.

Jana kulisambaa video fupi kwenye mitandao ya kijamii, ikimuonesha kijana wa Kitanzania akishambuliwa na mwanamama wa kichina, kwa madai ya kwamba alimfanyia vitendo vya udhadhalishaji wa kijinsia.

Taarifa iliyotolewa na Mwambata wa elimu Ubalozi wa Tanzania nchini China leo, imeeleza kuwa ubalozi huo umezungumza na serikali ya mji wa Xian na kuiomba mamlaka hiyo kuchukua hatua na kuhakikisha usalama wa Mtanzania huyo.

Pia ubalozi umeeleza kutoridhishwa na kitendo cha wananchi kujichukulia sheria mkononi, kwa kumpiga mtuhumiwa, huku ikiomba wahusika waliofanya kitendo hicho kuchukuliwa hatua  za kisheria.

“Ubalozi unaendelea kufanya mawasiliano na serikali ya mji wa Xian, kuhakikisha haki inatendeka na tunatoa rai kwa umma kuvuta subira, wakati suala hilo linafanyiwa kazi,” imesema taarifa hiyo.

Kijana huyo wa Kitanzania, ambaye hajafahamika kwa jina bado, anasoma chuo cha Xian Petroleum University nchini China.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad