Ubishi wa MZEE Wakulia..Kwanini Azam Wamechelewa Kumfukuza Kocha Moallin?


SIJASHANGAZWA. Nilipomuona mkurugenzi mtendaji wa Azam FC, Yussuf Bakhresa yuko bega kwa bega na timu nilijua tu lazima watu wakae kwa kutulia.

Ukiona Azam FC wanamsajili kipa ambaye aliwahi kucheza Ligi Kuu ya Ufaransa (Ligue 1) unajua kabisa Kocha Abdihamid Moallin maisha yake ndani ya timu yasingekuwa marefu.

Azam wamefanya usajili mkubwa ambao kila wakimtazama kocha Moallin wanamuona hatoshi.

Kuna kosa moja tu ambalo Azam FC wamefanya ni kuchelewa kuachana na Moallin. Ukitazama malengo ya Azam FC na uwekezaji wake unatarajia kumuona pia kocha mwenye uzito huo akiwa kwenye benchi.

Moallin sio kocha mbaya, lakini malengo ya Azam FC yanahitaji kocha mkubwa zaidi yake. Moallin sio kocha mbaya lakini usajili wa Azam FC unahitaji kocha mkubwa zaidi yake.

Kosa kubwa ambalo Azam FC wamefanya ni kuchelewa tu kumuondoa Moallin kwenye benchi la ufundi la kikosi cha kwanza.

Azam FC walitakiwa kuachana na kocha wao Moallin mara tu baada ya msimu uliopita kumalizika. Kitendo cha kuendelea kuwa na naye wakati wa dirisha la usajili, kwenda naye nchini Misri kwa maandalizi ya msimu mpya ni kosa kubwa.

Azam walipaswa kumtangaza kocha mpya mara tu baada ya msimu uliopita kwisha ili apate muda wa kusajili wachezaji. Ili apate muda wa kujiandaa.


Sina tatizo na Azam FC kumtimua kocha wao. Tatizo langu ni wao kufanya uamuzi kwa kuchelewa.

Kama Azam FC wana malengo ya kwenda kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara. Kama malengo ni kwenda walau hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika mabadiliko ya benchi la ufundi yalikuwa hayaepukiki. Lilikuwa ni suala la muda tu.


Kama Azam FC wangekuwa na lengo la kutengeneza timu yao bora ya baadaye kwa kutumia wachezaji wao wa ndani, kocha Moallin alipaswa kubaki kwa sababu hilo liko ndani ya uwezo wake.

Lakini kuipa timu ubingwa hayo ni maji marefu. Lakini kuipeleka timu
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad