Uhuru Kenyatta: ‘Rais wangu ni Baba (Raila Odinga)’



Rais Uhuru Kenyatta ameshikilia kuwa mrithi wake anayependelea bado ni kiongozi wa Azimio Raila Odinga.

Haya yanajiri licha ya uamuzi wa Mahakama ya Juu kuunga mkono kuchaguliwa kwa William Ruto mnamo Jumatatu, Septemba 5.

Kenyatta, akizungumza wakati wa mkutano wa viongozi waliochaguliwa katika muungano wa Azimio katika eneo la Masai Lodge katika Kaunti ya Kajiado leo, alisema kuwa nchi ingeelekezwa katika njia ifaayo Raila angechaguliwa kuwa rais.

“Mlijinyima fursa ya kuleta nchi pamoja, hamjamnyima Raila. Nilijitahidi kumfanyia kampeni,” Uhuru alisema.

Wakati huo huo, rais alithibitisha tena kuwa atakabidhi mamlaka kwa Rais mteule William Ruto mnamo Septemba 13 kwa mujibu wa Katiba.

"Nitakabidhi mamlaka nikitabasamu kwa sababu ni jukumu langu la kikatiba, lakini kiongozi wangu ni Baba [Raila Odinga]," Kenyatta alieleza.

Mkuu  huyo wa Nchi anayeondoka alitoa maoni yake kuhusu  muungano wa Azimio kumteua  Kenneth Marende kama mgombeaji wake wa kiti cha  Spika wa Bunge la Kitaifa, akiteuliwa na Farah Maalim  kama naibu wake na Kalonzo Musyoka kama Spika wa Seneti, akisaidiwa na Stewart Madzayo.

“Kalonzo Musyoka angekuwa Waziri Mkuu bora zaidi. Ninaamini pia angekuwa mwakilishi mzuri wa ajenda yetu katika Seneti,” alisema Kenyatta.

Wakati huo huo, Uhuru amewataka viongozi waliochaguliwa wa Azimio kuungana  akionya kuwa huenda wengine wakashawishika kujiunga na miungano mingine.

"Ikiwa ulichaguliwa kwa tikiti ya Azimio, shikamana na  na  Azimio usiyumbishwe. Je, utanunuliwa kwa shilingi tano au utasimama na Wakenya zaidi ya milioni 50?," Uhuru aliwauliza viongozi waliochaguliwa.

Kenyatta na Odinga wamehudhuria mkutano huo, pamoja na viongozi wengine wa  Azimio Martha Karua na Kalonzo Musyoka.

Kufikia sasa Rais Uhuru Kenyatta hajampongeza hadharani naibu wake William Ruto ambaye alitangazwa mshindi wa uchaguzi wa urais wa mwezi uliopita.

Makabidhiano ya mamlaka
Play video, "‘Nimetoa maagizo yote muhimu kwa makabidhiano ya mamlaka’ - Uhuru Kenyatta", Muda 2,30
02:30
Maelezo ya video,
‘Nimetoa maagizo yote muhimu kwa makabidhiano ya mamlaka’ - Uhuru Kenyatta

Rais Uhuru Kenyatta siku ya Jumatatu wiki hii alisisitiza kujitolea kwake kusimamia makabidhiano ya amani ya  mamlaka kwa utawala ujao.

Katika hotuba yake iliyopeperushwa kwenye runinga Jumatatu jioni, Uhuru alisema kwa kutii kiapo alichotoa alipochukua madaraka  cha kuzingatia sheria na kuheshimu maamuzi ya michakato ya mahakama, ataheshimu uamuzi wa Mahakama ya Juu zaidi wa kuidhinisha uchaguzi wa William Ruto kama Rais mteule.

Heshima kwa rais anayeondoka
th
Chanzo cha picha, Getty Images

Rais mteule William Ruto ameweka wazi maono yake ya Kenya ya kidemokrasia ambayo haina vitisho."Hii inaashiria mwisho wa siasa za udanganyifu, usaliti na ujanja," alisema Jumatatu baada ya mahakama ya juu kuishinisha ushindi wake .

"Tunataka siasa za Kenya za siku zijazo - kila kiongozi lazima ahukumiwe kwa kile anachosema na kile anachosema ndicho anachofanya."Bw Ruto anahisi kuwa yeye na wafuasi wake wakati fulani wamenyanyaswa.

"Tunataka kuwa na nchi inayozingatia utawala wa sheria - mfumo wa haki ya jinai utawekwa kwa ajili ya kupata wahalifu na uhalifu - hautatumika tena kwa sababu za kisiasa ... dhidi ya wale ambao wana maoni kinyume na yetu.

Pia ameshikilia kuwa Bw Kenyatta atatendewa vyema.

"Tutaheshimu rais wetu katika kustaafu kwake ... sisi ni watu wa heshima, sisi sio wadogo na hatuna wivu.Amefanya kazi nzuri na atakuwa na nafasi yake katika historia ya Kenya.

Hakuna mtu anayepaswa kushikilia chochote dhidi ya rais wa Kenya.

"Naye Bw Odinga ataheshimiwa' Ruto alisema

V
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad