UN: Hakuna dalili ya kumalizika kwa vita Ukraine

 


Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres amehutubia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, lililokutana kwa ajili ya kujadili kuhusu vita nchini Ukraine, na kuelezea masikitiko yake kuwa hakuna dalili za kusitishwa kwa mapigano kati ya nchi hiyo na Urusi.


Mkutano huo wa ngazi ya juu, unaongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa, Catherine Colonna kwa kuwa nchi yake ndio inashika urais wa Baraza la Usalama kwa mwezi huu wa Septemba, na kusema “Hali itazidi kuwa mbaya zaidi wakati majira ya baridi yanapokaribia, António Guterres ametabiri, hasa huku usambazaji wa gesi na umeme ukipungua.”


Katika miezi ya hivi karibuni, Guterres amebainisha “tumeshuhudia mateso na uharibifu usioelezeka. “Kama nilivyosema tangu mwanzo, vita hivi visivyo na maana vinaleta madhara makubwa kwa Ukraine na kwa ulimwengu wote. Wazo la mzozo wa nyuklia, ambalo haliwezi kufikiria, limekuwa mada ya mjadala.”


Almasi yetu si laana ni Baraka: Rais Masisi


Taswira ya ukumbi wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ambako wajumbe wamejadili amani na usalama Ukraine. Picha na UN.

Bodi ya maji yabaini chanzo kina cha maji kupungua

Amesema, mataifa yote, ambayo yana silaha za nyuklia, yanapaswa kuthibitisha kujitolea kwao kwa kutotumia na kuondoa kabisa silaha hizo, na kuongeza kuwa, “Umoja wa Mataifa umetoa msaada kwa karibu watu milioni 13 wenye uhitaji, ndani ya nchi ya Ukraine yenyewe na kwa wakimbizi ambao walijikuta katika nchi nyingine.”


Ameelezea pia wasiwasi wake, juu ya ripoti za mipango ya kuandaa “kura za maoni” katika maeneo ya Ukraine, ambayo hayako chini ya udhibiti wa serikali kwa sasa, akisema unyakuzi wowote wa eneo la jimbo na serikali nyingine kwa nguvu au kwa sababu ya tishio la serikali ni ukiukaji wa Mkataba wa Umoja na sheria za kimataifa.


Nchi wanachama, wa Baraza hilo la Usalama la Umoja wa Mataifa zikiwemo Ghana, Falme za Kiarabu, Gabon, Albania, Uingereza nazo zilikuwa ni miongoni mwa waliozungumza kulaani uvamizi wa Urusi na kueleza hakuna nchi ipo juu ya sheria na mikataba ya Umoja wa Mataifa inapaswa kuheshimiwa.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad