Unyama wa Hali ya Juu...Mzazi Amuua Mtoto Aliyemzidi Mwanaye Maksi Darasani


Mvulana mmoja mwenye umri wa miaka 13 amefariki baada ya kulishwa sumu na Mama wa Mwanafunzi mwenzake baada ya kumshinda katika masomo Shuleni eneo la Mji wa Pwani wa Karaikal Kusini mwa India.


Bala Manikandan ambaye alikuwa ni Mwanafunzi wa Darasa la 8, alishika nafasi ya kwanza katika masomo na shughuli za ziada Shuleni, jambo lililomkwaza Mama wa Mwanafunzi mwenzake ambaye kwa sasa amekamatwa kwa tuhuma za mauaji.


Siku ya Ijumaa, Mshukiwa aliyetambulika kwa jina la Sahayarani Victoria, alidaiwa kujifanya Mama Mzazi wa Bala na kwenda kumfuata katika mlango wa Shule hiyo na kumkabidhi Kijana huyo chupa iliyokuwa na kinywaji.


Kijana huyo alikuwa akijiandaa kutumbuiza kwenye hafla ya kitamaduni ya siku ambayo hufanyika kila mwaka katika shule hiyo na ndipo alipokunywa kinywaji hicho ambapo muda mchache akaanza kujisikia vibaya, kutapika kabla ya kufariki jumamosi usiku.

SOMA PIA: Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo

Wazazi wa Bala waliwasilisha malalamiko katika Kituo cha Polisi cha eneo hilo baada ya kanda ya CCTV kumuonesha Victoria akimwomba Mlinzi ampelekee mvulana huyo chupa hizo, Madaktari wamesema Mvulana huyo alifariki kutokana na kukosa hewa baada ya chembechembe za chakula kuingia kwenye mfumo wake wa upumuaji.

 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad