Uongozi wa Simba Wafunguka Hatma ya Mchezaji Mzungu Serbia Dejan Georgijevic



Uongozi wa Simba SC umesisitiza kuendelea kutambua na kuheshimu mkataba uliopo kati yake na Mshambuliaji kutoka Serbia Dejan Georgijevic, aliyesajiwa mwanzoni mwa msimu huu akitokea Klabu ya Domžale ya Slovenia.

Akizungumza kwa niaba ya Uongozi wa Simba SC wakati wa mahojiano na Kituo cha Radio cha Wasafi FM kupitia Kipindi cha Sports Arena leo Ijumaa (Septemba 16), Meneja wa Kitengo Cha Mawasiliano na Habari Ahmed Ally amesema, Dejan ni Mchezaji halali wa klabu hiyo na Mkataba wake utaendelea kuthibitisha hilo.

Ahmed amelazimika kulizungumza hilo baada ya kuulizwa kuhusu hatma ya Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 28, ambaye alionekana kupewa nafasi ya kucheza kwa dakika kadhaa wakati wa Kocha Zoran Maki, lakini kwa sasa imekua tofauti.

Amesema Dejan ataendelea kusalia Simba SC, licha ya kuonekana kutopata nafasi ya kuanza ndani ya Kikosi Chao, kwa sababu mpango wa kucheza ama kutokucheza upo chini ya Benchi la Ufundi ambalo kwa sasa linaoongozwa na Kocha Juma Mgunda akisaidiana na Seleman Matola.

Amesema kwa sasa Mshambuliaji huyo Ndiye Mchezaji mwenye Mkataba mrefu zaidi ndani ya Simba SC na kwenye Usajili wake ulikuwa ni pendekezo la Uongozi na sio Kocha Zoran Maki kama inavyosemwa na wengi.

Hadi sasa Dejan ameshaifungia Simba SC bao moja kwenye Mshike Mshike wa Ligi Kuu Tanzania Bara, akifanya hivyo katika mchezo dhidi ya Kagera Sugar uliopigwa mwishoni mwa mwezi uliopita Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Katika mchezo huo Simba SC ilishinda mabao 2-0, bao la Kwanza likifungwa na Mshambuliaji kutoka nchini Zambia Moses Phiri.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad