Vyuo vyatakiwa kubadili mitaala kuendana na wakati

 


Wizara ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari imevitaka vyuo vinavyofundisha masomo ya TEHAMA kufanya mabadiliko ya mitaala yao, ili kuzalisha vijana watakaokuwa na ushindani kwenye soko la ajira, ndani na nje ya nchi.


Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Mathew katika maadhimisho ya Miaka kumi Ndaki ya Tehama ya Chuo kikuu cha Dar es Salaam  ( CoICT), huku akikiagiza chuo cha Dar es Salaam kuongeza kozi zinazoendana na wakati wa sasa.

Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Prof. William Anangisye

amewataka wahadhiri wenye sifa kujitahidi kufanya tafiti ili kuongeza idadi ya maprofesa nchini, huku akisisitiza wasomi wa TEHEMA kutumia maarifa yao kutatua changamoto zilizopo kwenye jamii.

Naye RASI (Principal) wa CoICT Prof. Joel Mtebe amebainisha kuwa miongoni mwa changamoto zinazowakabili ni mtandao (internet) ya uhakika chuoni hapo, jambo linalowakwamisha wanafunzi katika masomo yao.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad