Wafahamu Hilal Wapinzani wa Yanga kwenye Hatua ya kwanza




Imeandikwa na @gharib_mzinga23 📌

Hawa ndio wafalme wa Soka la Sudan, Ndio klabu iliyobeba mataji mengi zaidi nchini humo na Ndio Wawakilishi Bora zaidi wa CECAFA kwenye CAF.

Hilal imeshacheza Fainali za CAF mara 2 zote Ilipoteza, Ilikua 1987 Kwa Ahly ya Misri na 1992 Kwa Wydad Casablanca ya Morocco.

Imecheza nusu Fainali ya michuano ya CAF mara nyingi zaidi ya klabu yoyote ya CECAFA, ikifanya hivyo mara 5, Robo Fainali nyingi.

Makundi 'Business as usual' Mara mwisho Msimu Jana, 2021/22, Hilal Kwa Sasa Wana nguvu ya Kiuchimi. Kwanini ?

Wana kikosi kinachokaririwa kua na thamani ya Dola za marekani $ Million 2.75 zaidi ya Tsh Bilioni 6.3.

Baada ya Misimu kadhaa kutofanya makubwa kimataifa, Hilal Walimuomba Tycoon, Bilionea Turk El Sheikh wa Saudia Arabia kua raisi wa heshima wa klabu hiyo.

Huyu Mwamba ndiye aliyeinunua Pyramid FC ya Misri kutoka Al Assiyout kitaka kuifanya klabu hatari zaidi Misri na Afrika, Baadae akaiuza.

Mwamba huyu anayemiliki klabu ya Almeria ya Hispania aliweka mzigo Kwa kuongeza nyota wenye uwezo ili Hilal ifanye vizuri zaidi Afrika.

Aliingia Msimu uliopita ila Msimu huu akaweka Mkwanja, Ambao Umenunua Nyota wengi kama Issa Fofana kutoka San Pedro ya Ivory Coast, Cloud Singone kutoka Asec Mimosas ya Ivory Coast pia.

Imoro Ibrahim kutoka Asante Kotoko ya Ghana, John Mano(aliwafunga Simba, Kirafiki), Makabi Lilepo kutoka DRC, Lamine Diedhou kutoka Senegal.

Wakarudisha mtambo wao wa mabao Waleed Bkhet aliyekua Kuwait akitoke Hilal na amerejea tena.

Kama haitoshi Kocha mwenye taji la Shirikisho Afrika Msimu Jana Frolent Ibenge wa DRC. Mpango wao ni Operation Semi Finals, Next destination is Jangwani.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad