Siku ya Ijumaa, Septemba 2, Jaji Mkuu Martha Koome alisema kuwa atatangaza saa ambapo majaji wa Mahakama ya Upeo intarajiwa kutoa uamuzi kuhusu kesi ya urais
Hata hivyo, Jumatatu asubuhi, Septemba 5, Koome hakuwa ametangaza ni saa ngapi atatoa uamuzi na kusababisha Wakenya mitandaoni kuingiwa na wasiwasi.
Ili kutuliza nyoyo za Wakenya wengi, mahakama hiyo ilibainisha kwamba itatangaza uamuzi huo kufikia saa sita mchana
Siku ya Ijumaa, Septemba 2, Jaji Mkuu Martha Koome alisema kuwa atatangaza saa ambapo majaji wa Mahakama ya Upeo intarajiwa kutoa uamuzi kuhusu kesi ya urais.
Mahakama ya Upeo: Wakenya Waishiwa na Subira ya Kujua ni Saa Ngapi Kesi ya Urais Itaamuliwa
Jaji Mkuu wa Mahakama ya Upeo Martha Koome. Picha: UGC.
Hata hivyo, kufikia saa tatu asubuhi, Jumatatu, Septemba 5, Koome hakuwa ametangaza ni saa ngapi atatoa uamuzi na kusababisha Wakenya mitandaoni kuingiwa na wasiwasi.
Ili kutuliza nyoyo za Wakenya wengi, mahakama hiyo ilibainisha kwamba itatangaza uamuzi huo kufikia saa sita mchana, kupitia ukurasa wake rasmi wa Twitter.
Awali mahakama ilisema:
"Kesi ya urais: Mara tu baada ya Mahakama ya Upeo itabainisha saa ya kutoa uamuzi, tutapakia hapa," ujumbe huo wa Twitter ulisoma.
Huku akidadavua suala hilo, wakili wa jiji Ahmednasir Abdullahi alidai kwamba, huenda ikawa kuchelewa kwa kutangazwa kwa saa mahsusi kumesababishwa na Koome kukabiliana na maoni yaligawanyika kutioka kwa majaji wengine.
"Sababu moja ya Jaji Mkuu kukosa kuwaambia Wakenya ni saa ngapi uamuzi ya kesi ya urais utatolewa na Mahakama ya Upeo kwa Wakenya na dunia nzima, ni kuwa huenda anakabiliwa na maoni yaliyogawanyika kutoka kwa majaji wengine saba na anajaribu kuwafanya watoe kauli moja," Ahmednasir alisema.
Zifuatazo ni baadhi ya jumbe zilizoonekana Mtandaoni:
Titus Chefyekei alisema:
"Uamuzi huo unapaswa kutolewa jioni wakati kila mtu amewasili nyumbani."
Michael Ndonye alisema:
"Wakenya nendeni kazini! Majaji wa Mahakama ya Upeo wana hadi saaa sita za usiku kutoa uamuzi utakaochukua dakika 30."