Watalii hao wanaripotiwa kuonekana wakiomba katika mitaa ya Old Town na Soko la Marikiti huko Mombasa Kenya.
Raia hao 40 wa Jordan, ni wakiwemo watu wazima 19 na watoto 21 ambao walikuwa na hati halali ya kitalii
Uchunguzi wa polisi ulifichua kuwa raia hao walikuwa wakielekea Eastleigh jijini Nairobi na ilibidi waombe pesa za kusafiri.
Polisi katika kaunti ya Mombasa wanawazuilia watalii 40 raia wa Jordan baada ya kupatikana wakiombaomba mitaani mjini humo.
Kamanda wa Polisi wa Kaunti Ndogo ya Mvita Maxwell Agoro anazungumza na mmoja wa raia 40 wa Jordan waliokamatwa.
Kamanda wa Polisi wa Kaunti Ndogo ya Mvita Maxwell Agoro akizungumza na mmoja wa raia 40 wa Jordan waliokamatwa.
Watalii hao wanaripotiwa kuonekana wakiomba katika mitaa ya Old Town na Soko la Marikiti Alhamisi iliyopita ili kutafuta pesa za kufadhili ziara yao ya Nairobi.
Akithibitisha kukamatwa kwao, Kamanda Mkuu wa Polisi wa kaunti ndogo ya Mvita, Maxwell Agoro alisema polisi waliwakamata watalii hao baada ya kudokezwa na wakazi.
Kulingana na Agoro, 40 hao, ni wakiwemo watu wazima 19 na watoto 21 ambao walikuwa na hati halali ya kitalii, lakini kuombaomba kulikiuka masharti ya hati zao za kusafiria, na kupelekea kukamatwa kwao.
Kisii: Mama na Bintiye Wanaswa Wakisakata Densi Kwenye Kaburi la Pasta Usiku
“Baada ya kuwapata, polisi waliwasindikiza hadi kituo cha polisi cha Central kwa mahojiano. Walipatikana wakienda kinyume na udhibiti wa visa kwa kujigeuza ombaomba kinyume na kuwa watalii,” akasema Agoro kama alivyonukuliwa na Nation.
Agoro aliongeza kuwa uchunguzi ulifichua kuwa raia hao 40 wa kigeni walikuwa wakielekea Eastleigh jijini Nairobi na ilibidi waombe pesa za kusafiri.
Raia hao wanatarajiwa kupelekwa afisi za idara ya uhamiaji ili hatua zaidi kuweza kuchukuliwa.
Kwa sasa wanazuiliwa katika Makao Makuu ya Polisi yaMkoa wa Pwani ambapo wanaendelea kuhojiwa.
Wakenya waonywa kusafiri Saudi Arabia
Katibu Mkuu wa Wizara ya Masuala ya Kigeni Macharia Kamau alisema Wakenya hupuuza onyo dhidi ya kusafiri Saudi Arabia.
Kamau alikuwa anajibu swali la mwanamtandao aliyetaka kujua juhudi za serikali za kumaliza visa vya wanawake kuteswa katika taifa hilo la Uarabuni.
"Tafadhali. Tumewaambia Wakenya mara kwa mara waache kutuma vijakazi Saudi. Mmechagua kutosikiliza," alisema Kamau.
Justina Wamae Afichua Manifesto ya Roots Party Ilimsabibishia Mzozo na Wazazi Wake: "Betri za Fisi Au Bangi?"
Hii ni kufuatia masaibu ya Diana Chepkemoi, ambaye alikuwa akidhulumiwa na bosi wake Mwarabu, kusambaa kwenye mitandao ya kijamii.