Waziri aanika chanzo mfuko NHIF kuyumba



Dar es Salaam. Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ametaja chanzo cha kuelemewa kwa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) akisema magonjwa yasiyoambukiza, urasimu na kuingizwa kwa wasio watumishi wa umma ambao asilimia 99 ni wagonjwa.

Waziri Ummy ameyasema hayo leo Alhamisi Septemba Mosi, 2022 wakati akitoa ufafanuzi kuhusu huduma na madai ya kuyumba kwa mfuko huo jijini Dodoma ku.

“NHIF imeanzishwa mwaka 2001 kuwahudumia watumishi wa umma pekee, lakini kutokana na wananchi walihitaji kuingizwa, Serikali ilifanya marekebisho ya mara kwa mara tuliruhusiwa kuingiza watu ambao si watumishi na hapa ndipo chanzo cha tatizo,” amesema na kuongeza;

“Tukibakiza watumishi wa umma pekee hakutakuwa na shida lakini changamoto imekuja baada ya kuingizwa wa hiari ikiwemo Toto Afya Card, asilimia 99 ya watoto waliojiunga tayari ni wagonjwa na wengine mtoto yupo hospitali anahitaji upasuaji ndiyo anaingizwa.”


Amesema watoto walio katika umri wa miaka 18 wanaostahili kuingia katika mfumo huo wanakadiriwa kuwa milioni 20 lakini mpaka sasa waliojiunga ni 185,000 pekee ambao asilimia 99 yao ni wagonjwa.

Ametaja chanzo kingine kuwa ni watumishi wa NHIF kujiingiza katika tabia za udanganyifu wakishirikiana na vituo vya kutolea huduma za afya.

“Lakini hapo katika suala jingine inasemwa huko kwamba NHIF mnashirikiana na vituo vya kutoa huduma za afya katika kukuza madai chunguzaneni hilo na bananeni wenyewe ndani huko,” amesema Waziri Ummy.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad