Akizungumza Wema ambaye ni mhamasishaji wa chanzo ya UVIKO-19 anasema kuwa, anaufurahia mno mwezi huu kwa sababu baadhi ya vitu vyake vinakwenda sawa kama anavyotaka na alivyopanga, kiufupi anasema Mungu amemtendea miujiza.
“Jamani mniache tu, huu ni mwezi wangu jamani, Mungu amenitendea mambo mengi mwaka huu, ni mwaka wangu huu hivyo waniache tu niinjoi mimi,” anasema Wema ambaye anatarajia kufanya pati kubwa ya kumbuziki ya
kuzaliwa ifikapo Septemba 28, mwezi huu ambapo atakuwa anatimiza umri wa miaka 31.