Wivu wa Mapenzi, Ushirikina Vyatajwa Sababu za Mauji


Wakati kumekuwa na wimbi la mauaji nchini, Serikali imesema sababu za wananchi kujichukulia hatua mkononi ni wivu wa mapenzi, migogoro ya ardhi, ulevi na imani za kishirikini.

#Dodoma. Wakati kumekuwa na wimbi la mauaji nchini, Serikali imesema sababu za wananchi kujichukulia hatua mkononi ni wivu wa mapenzi, migogoro ya ardhi, ulevi na imani za kishirikini.

Kauli hiyo imetolewa baada ya swali lilioulizwa leo Jumatano Septemba 14, 2022 na Mbunge wa Viti Maalum, Cecilia Pareso ambaye ametaka kufahamu nini kauli ya Serikali katika kutatua changamoto ya wimbi kubwa la mauaji hapa nchini Tanzania.

Akijibu swali hilo kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Ndani, Naibu Waziri katika Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Hamad Hassan Chande, amesema ni kweli kumekuwa na ongezeko la matukio ya mauaji hapa nchini.

“Matukio mengi yanasababishwa na wananchi kujichukulia sheria mkononi, wivu wa mapenzi, migogoro ya ardhi, ulevi na imani za kishirikina,”amesema.

Amesema katika kudhibiti wimbi hili waliunda timu maalum ya kuchunguza na kutoa mapendekezo ya hatua za kuchukua.

Chande amesema pamoja na kuchukua hatua za kisheria kama zilivyopendekewa na timu waliyoiunda, Serikali kupitia Jeshi la Polisi imeendelea kutoa elimu kwa wananchi.

Amesema elimu hiyo imekuwa ikitolewa kwa kuwashirikisha viongozi wa siasa, dini, wazee wa mila na watu wanaoheshimika kufuata sheria, kanuni na taratibu za nchi, katika kutatua migogoro na migongano katika jamii.

Baada ya majibu hayo, Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson amesema licha ya Serikali kuchukua hatua bado linaendelea kukuwa.

“Sasa sijui kwamba ni kwasababu polisi ndio wanaoviambia vyombo vya habari, kwa hiyo inakuwa ni habari nzito fulani. Hivi mwingine ambaye anajua kuwa hilo jambo haliwezekani anafikiri kuwa na mimi naweza kulifanya,”amesema.

Spika ameitaka Serikali kuangalia hatua za kawaida na kwamba pengine matangazo nayo yanaleta hiyo changamoto.

“Na mtuulize sisi watu wa kawaida kabisa tunafikiri hilo.

CHANZO MWANANCHI

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad