Karibu watu 75 wamefariki dunia baada ya daraja kuporomoka nchini India, wakati ambapo karibu watu 500 walikuwa wakiadhimisha sherehe za kiimani za Diwali kwenye daraja hilo, na maeneo ya karibu wakati nguzo zilizokuwa zinalishikilia zilipokatika.
Waziri wa serikali ya mkoa wa Gujarat, linapopatikana daraja hilo, Brijesh Merja amesema pamoja na vifo hivyo, bado kuna wengine wengi waliozama majini na wengine 80 tayari wameokolewa.
Waokoaji wakiendelea na shughuli za utafutaji wa miili baada ya daraja lililovuka mto Machhu, kuporomoka huko Morbi, takriban kilomita 220 kutoka Ahmedabad, mapema Oktoba 31, 2022. watu 75 walifariki Oktoba 30 nchini India baada ya daraja hilo la zamani la watembea kwa miguu la enzi za ukoloni lililojengwa mika 150 iliyopita kuporomoka, na kusababisha watu wengi kutumbukia mtoni chini. Picha: Sam Panthaky / AFP.
Daraja hilo la Machchhu, lililojengwa karibu miaka 150 iliyopita lina urefu wa karibu kilomita 200 na lilifunguliwa siku ya Jumatano baada ya kufungwa kwa miezi saba kwa ajili ya matengenezo.
Hata hivyo, lilifunguliwa kabla ya kupata cheti cha idhini ambapo Waziri mkuu wa India, Narendra Modi ametangaza familia za wahanga kulipwa, wakati operesheni za uokozi zikiendelea.