Achomwa vibaya na Uji kisa Kala Maharage kijiko kimoja, Shangazi ahusishwa kufanya tukio hilo




Mwanamke  mmoja anaefahamika kwa jina la Violet Masawe mkazi wa mtaa wa Bogini  Wilayani  Moshi Mkoani Kilimanjaro anashikiliwa na Jeshi la  Polisi kwa tuhuma za kumchoma kwa uji wa  moto mtoto wa kaka yake aliyetambulika kwa jina la Elvis Shoo mwenye umri wa miaka 27.

Inaelezwa kuwa  kuwa Kijana Elivis alichukua kijiko cha maharage na kula pasipo kumhusisha shangazi yake ndipo yalipotokea majibizano yaliyopelekea  kijana huyo kumwagiwa uji wa moto tukio ambalo limemsababishia  kupata Majeraha  katika  Maeneo ya mwili wake ikiwemo eneo la shingoni na hivi sasa  amelazwa katika hospitali ya Pasua mjini Moshi kwaajili ya kupatiwa Matibabu.

Kwa taarifa kamili unaweza ukabonyeza play kufahamu zaidi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad