Afrika Hakuna Aliyevunja Rekodi ya Calm Down ya Rema na Selena Gomez, Ule Wimbo Aliyoshirikishwa Mondi na Muhindi sio wa Afrika


Ebu tuache kuchekesha umati kwa kutafuta rekodi za kuokota okota, Bongo Flava au jina la msanii halijengwi hivyo. Hivi aliyewaambia JUGNI imevunja Rekodi ya Rema ni nani, na kupitia nini, saa ngapi na wapi? Mbona tunafosi vitu bila kujua kutofautisha ulinganifu wa vitu vyenyewe! Rekodi ya Rema ni Afrika na itabaki hivyo, kama JUGNI imevunja rekodi ya Rema, hizo nyimbo za BTS tusemaje?. Tunapenda wasanii wetu wafike juu zaidi kimafanikio katika muziki wao, ila sio kwa hii staili, na ndio maana hizi rekodi tunabaki nazo wenyewe huku kwetu, mara Views Milioni kwa sekunde mara flani kuvunja rekodi,mara albamu ya flani imeshika No. 1 Apple music duniani🤔.


Calm down Remix ni Afrobeats music, Ni wimbo wa Rema x Selena Gomez, haijalishi upo kwenye YouTube Channel ya nani. Selena Gomez kawa featured na kaingia mazima kwenye Afrobeats version, JUGNI ni Punjabi version, haina hata chembe ya muziki wa Afrika, pia ni wimbo wa Diljit Dosanjh x Diamond na upo kwenye YouTube Channel ya Dosanjh, na ni wimbo ulio nje ya bara la Afrika.


Kwanini tunasema Rema kaweka rekodi ya kufikisha views Milioni 3+ ndani ya masaa 24 barani Afrika?, ni kwasababu ni wimbo wa kwanza wenye mahadhi ya kiafrika, uliozaliwa barani Afrika kufikia viwango hivyo kwenye mtandao wa Youtube, na ndio Maana Calm down remix ilishindanishwa na rekodi ya Buga. Sio kuwa miziki nje ya bara la Afrika haifikii hizo rekodi, zinawekwa sana na imekuwa kawaida kwao, hasa msanii wetu kaimba kihindi japo kwa Lugha ya kiswahili, kashirikishwa na muhindi kwenye account ya muhindi, na muziki ni nje ya bara la Afrika, anapewa heshima ya kuvunja rekodi kwenye muziki wa Afrika, hivi tuko serious kweli?

Darasa hili linahitaji watu ambao akili zao hazijachoka, Futeni ubao mapema tayari kwa somo lijalo.

NB: Tusilazimishe Chokaa kuwa rangi, na tui la karanga kuwa la Nazi.

By Sajomedia

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad